Habari zenyewe kwa utendeti

4 Mar 2014

Basi jamaa mmoja kaingia kinyozi huku akiwa ameandamana na mtoto.

Baada ya kunyolewa, akamwambia yule mwenye kinyozi, "Hebu mnyoe huyu mtoto. Naenda huku dukani kununua vitu mbili, tatu."

Basi mwenye kinyozi akamketisha mtoto na kumnyoa.

Baada ya muda wa masaa mawili hivi, yule jamaa bado hajarejea.

Mwenye kinyozi akamuuliza yule mtoto, "Huyu babako anarudi saa ngapi?"

Mtoto akamjibu, "Yule si babangu. Nimekutana tu naye hapa nje akaniambia tuje hapa tunyolewe bure."

Duh!!!

JOIN GROUP KENYA


 

ADVERTISEMENTS