Taarifa: Masaibu ya walevi nchini Kenya

17 Mar 2014

Basi mlevi mmoja kaoa mke mbadhirifu...

Mkewe hakuweza kutulia kwenye ndoa hata siku moja.

Siku moja mkewe akiwa anajivinjari na msela, mlevi akarudi nyumbani bila kutarajiwa.

Mke yule mkewe akamwambia msela, "Usiondoke, lala hivo hivo. Mume wangu mlevi hatagundua."

Msela akalala na kutulia tuli.

Naye mlevi akiwa chakari, akapanda kitandani mle. Wote watatu wakalala... Baada ya muda kidogo mlevi akagutuka, akagundua utofauti pale kitandani, akahesabu miguu na kuona ipo sita, akamtikisa mkewe, "Ala! Mke
wangu, mbona miguu ipo sita nani kalala hapa?"

Mkewe akamjibu kwa ukali, "Toka hapa na ulevi wako, miguu sita itoke wapi hebu shuka kitandani uhesabu vyema!"

Mlevi akashuka, akahesabu kwa sauti, "MOJA... MBILI... TATU... NNE... AHAA KUMBE KWELI NILIKOSEA KUHESABU, SAMAHANI MKE WANGU."

Nami nikiwa tu naskia matukio huku nimejificha karibu na dirisha lao, bedroom.

By: Eliud Karimi

JOIN GROUP KENYA


 

ADVERTISEMENTS