The older you get, the wiser you become

24 Mar 2014

Mkulima mmoja alikuwa anafuga kuku wa kienyeji.

Alikuwa na majike 25 na jogoo mmoja. Baada ya kuona jogoo amekuwa mzee akaamua kununua jogoo mwingine. Lile jogoo jipya kufika tu, kukawa na mazungumzo kati yake nation yule jogoo mzee:

JOGOO MZEE: Karibu dogo, karibu sana nadhani tutashirikiana vizuri ili kuhakikisha hawa kuku wanataga mayai.

JOGOO DOGO: Wewe umeshazeeka ndio maana nimeletwa mimi damu mpya. Hakuna kushirikiana wala nini umekwisha wewe.

JOGOO MZEE: Kama unaona nimekwisha basi tufanye mashindano unipime.

JOGOO DOGO: Mashindano gani?

JOGOO MZEE: Tushindane mbio tuzunguke nyumba mara mbili, ukishinda mi najitoa. Ila kwa kuwa mi mzee naomba uniache nianze kama hatua kumi mbele.

JOGOO DOGO: Sawa basi. Haya anza kukimbia.

(Mbio zikaanza, walizunguka nyumba mara moja tu, mkulima akamfwata yule jogoo mdogo akamkamata na kumchinja huku akilalamika)

MKULIMA: Yaani dunia imeharibika, huyu Jogoo wa sita sasa namnunua badala ya kufukuza majike analeta ushoga hapa! Anataka kupanda jogoo mwenzake badala ya KUKU!

Labda ahamie huko kwa Obama. Hapa Sitaki Huo upuuzi!

Say what?!

JOIN GROUP KENYA


 

ADVERTISEMENTS